RITA - UTARATIBU WA KUHAKIKI VYETI VYA KUZALIWA NA VlFO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU 2018/2019
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuwafahamesha waombaji wa Mikapo ya Wanafunzi wa El1mu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa zoezi la Uhaklki wa Vyeti vya Kuzaliwa kwa waombaji, na vyeti vya vifo vya wazazi wa waombaji nchi nzima kama ambavyo tumekubaliana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elrmu ya juu (HESLB) linaendelea kwa njia zifuatazo:- Mwombaji kuwasilisha nakala ya cheti katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya alikopata cheti cha Kuzaliwa;
- Waombaji wanaoishi nje ya Wilaya walikopata Cheti cha Kuzaliwa pamoja na waliopo Mkoa wa Dar es Salaam waingie katika mtandao kwa anwani:- http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki, ,ili kupata maelezo ya jinsi ya kutuma nakala ya Cheti na Risiti ya malipo. Baada ya uhakiki cheti kilichohakikiwa kitatumwa kupitia anwani ya mwombaji katika mtandao.
Kila mwombaji awasilishe/atume kivuli cha cheti inayosorneka vizuri kwa ajili ya uhakiki ikiambatamshwa na nakala ya Risiti ya malipo. Vile vile, utaratibu uliotaja hapo juu utatumika kwa ajlli ya kuhakiki vyeti vya vifo vya wazazi.
Aidha. Tunapenda kuwasisitiza waombaji wote kufuata utaratibu ulioelekezwa hapo juu ili kuepuka usumbufu.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0800117482
lmetolewa na:
Emmy Kalomba Hudson
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu • RITA
Tovuti ya Uhakiki wa Vyeti ya RITA